Sakata wagonjwa kuwekewa damu ya VVU

21Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Sakata wagonjwa kuwekewa damu ya VVU

BAADA ya sakata la mtu kufa kwa kuwekewa damu chafu hospitalini Uingereza, serikali imeamua kurudisha nyuma mikono ikikiri uchafu huo wa damu iliyokuwa na virusi vya maradhi mbalimbali, ikiwamo Ukimwi na imeuomba umma msamaha.

Sasa serikali inaandaa timu maalumu ya uchunguzi kupata undani wa sakata hilo, ambalo msukumo wake ulipata moto zaidi mwaka jana.

Katika sakata hilo lililotokea mwaka jana, wanaharakati wanakuja juu wakidai watu 2,400 wamekufa kutokana na kupewa damu hiyo chafu yenye virusi tangu zama za miaka ya 1970 na 1980, huku kukiwepo madai kuna damu iliyotolewa nje ya nchi na nyingine magerezani.

Mlalamikaji Carol Grayson, anadai mumewe aitwaye Peter, alikufa kutokana na kupewa damu hiyo muongo mmoja uliopita, lakini sakata hilo ndiyo sasa inaibuliwa rasmi, baada ya kupiganiwa na walalamikaji kwa muda mrefu uliotajwa.

"Niliamua kuacha kazi ili kumhudumia mume wangu kwa miaka mingi na sikuweza kupata watoto, kwa sababu wakati nadhani nipate ujauzito, nikatahadharishwa naweza kimuathiri mtoto. Ushauri niliyoupata wakati huo, nisipate mtoto. Kwa hiyo kuna ujumbe mkubwa kuhusiana na familia. Haimuathiri mtu tu, bali famia yote,” analalamikka mweanamke huyo.

"Nilichukia sana kuchaganyikiwa kwelikweli na kuweza kuamini kila kilichonijia mawazoni. Unajua haya ya demokrasia na haki, ni uongo tu,” anaendelea kulalamika mwanamke huyo.

Mwezi Julai mwaka huu, Waziri Mkuu wa Uingereza, aliagiza kuundwe chombo huru kuchunguza sakata hilo, ikiwahusisha wahusika wa afya kujibu yatikayo katika msukumo wa malalamiko nchini humo

Msemaji wa Wizara ya Afya nchini Uingereza, anafafanua: “Sakata la damu iliyoathiri katika miaka ya 1979 na 80 ni baya sana na serikali imetangaza tume huru kuwahoji waathirika, kuhakikisha kwamba waathirika na familia zao hatimaye wanapata majibu, kwani wametumia miongo (kadhaa) kusubiri.”

 

Habari Kubwa