N'Zonzi anavyovuta  nyomi usajili Januari

01Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
N'Zonzi anavyovuta  nyomi usajili Januari

“MUSTAKABALI wangu wa baadaye ni wazi naondoka Seville," Steven N'Zonzi aliweka bayana. "Kitu pekee ambacho kinanihuzunisha ni namna ninavyomaliza.”

" Steven N'Zonzi.

Kutokana na kauli hiyo kutakuwa na klabu nyingi ambazo zitahitaji huduma yake. Amekosa nafasi chini ya kocha wa Sevilla, Eduardo Berizzo, na inaonekana sasa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28, sasa anapatikana kwa pungufu ya bei.

Hapatakuwa na uhaba wa timu zinazovutiwa na huduma yake, na tangu akiitumikia Blackburn chini ya Sam Allardyce, N'Zonzi alijijengea jina yeye binafsi kama kiungo bora na kuzivutia klabu nyingi Ulaya.

Hapa ni makazi saba ya klabu ambazo kiungo huyo raia wa Ufaransa anaweza kwenda kutoa huduma...

7. ArsenalKwa mara nyingine N'Zonzi amehusishwa na kujiunga na Arsenal katika wiki za hivi karibuni, na hakuna la kushangaza.

Kiungo huyo mwenye nguvu, ataweza kutoa huduma ambayo 'The Gunners' imekuwa ikiitafuta kwa muda mrefu. Ingawa pia yupo mbali sana pindi linapokuja suala uwezo wa kupasua safu za ulinzi.

N'Zonzi pia ni hodari mzuri wa kutoa pasi za kufika, uwezo wa kutuliza mechi ya presha na atamudu vema staili ya uchezaji wa miamba hiyo Emirates.

Kufuatia taarifa kwamba alikuwa London hivi karibuni, inawezekana Arsenal imepiga hatua haraka ya kumnasa. Dau linalohitajika ili kuvunja mkataba wake ni pauni milioni 35, ambazo zinalipika.

6. EvertonEverton, ambayo inajipanga kujiimarisha chini ya Sam Allardyce, pia imekuwa ikihusishwa na N'Zonzi.Kiungo huyo wa Sevilla, hivi karibuni alicheza chini ya Allardyce akiwa Blackburn, na sasa anaweza kutakiwa tena na kocha wake huyo wa zamani. 

Kocha huyo wa Everton ni shabiki mkubwa wa N'Zonzi. Pia aliripotiwa kuangalia uwezekano wa kiungo huyo kuichezea England wakati akiinoa timu hiyo ya Taifa.

Kutokana na hilo, pamoja na Everton kuhitaji kujiimarisha, N'Zonzi anaweza kuwa windo muhimu kwa 'Toffees' hao.

5. RomaInaonekana haiepukiki kwa Roma kuvutiwa na N'Zonzi. Na hilo ni kwa sababu klabu hiyo ya Serie A ilimsajili Monchi katika majira ya joto, mkurugenzi huyo wa soka alikuwapo Sevilla kipindi chao cha mafanikio Italia.

Monchi atakuwa anamjua N'Zonzi vizuri; na ubora wake wa kuvutia wakati akiwa katika klabu hiyo miaka miwili iliyopita.

Na kwa uelewa huo utakuwa unatosha kumvutia kuungana naye tena. Utakuwa ni wasifu wakuvutia kwa N'Zonzi, na atafanya kazi vizuri katika mfumo wa kocha Eusebio Di Francesco.

4. LiverpoolLiverpool inaonekana kujiandaa kumpoteza Emre Can, na haraka itakuwa ikimtazama N'Zonzi kama mbadala.Mfaransa huyo anaweza kucheza soka la presha kubwa chini ya Jurgen Klopp, na pengine anaweza kuongeza umoja kwa wakati Liverpool inapouhitaji mbele. 

Kama Liverpool itainasa huduma ya N'Zonzi, ni jambo linalosubiriwa kuonekana, ingawa litakuwa suala la kushangaza kuiona ikimnasa wakati huu klabu kibao za Ligi Kuu England zikivutiwa naye.

3. JuventusKulikuwa na taarifa majira ya joto kuwa N'Zonzi amekubali kusaini mkataba na mabingwa wa Serie A, Juventus, ingawa dili hilo halikuiva.

Lakini kuvutiwa kwao hakuwezi kuwa kumetoweka kabisa. Kama Juventus bado inahitaji kiungo, wazo la kumnasa N'Zonzi linaweza kuwa sahihi.

2. Leicester“Ninaipenda Ligi Kuu England," N'Zonzi alisema. "Ukweli ninaipenda Ligi Kuu England, hapa ndipo nilipoanzia kwa kuwa katika kiwango kizuri."

Kama unashangaa kwa nini kuna klabu nyingi za Ligi Kuu England zilizojumuishwa katika orodha hii, hiyo ni sehemu ya sababu. N'Zonzi ni mshirika mzuri wa soka la England kutokana na historia yake na klabu za England kuonekana kumpenda pia.

Kulikuwa na tetesi za Leicester kumfuatilia majira ya joto, lakini kwa sasa itakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa baadhi ya klabu, kama itarudia lengo lake hilo. 1. BarcelonaKiwango cha kuvutia cha N'Zonzi kimetua La Liga, hivyo inaeleweka kuwa klabu katika daraja hilo zitakuwa tayari zimeshaweka kumbukumbu.

Kulikuwapo na tetesi mwaka uliopita kuwa Barcelona, imemmulika kiungo huyo wa zamani wa Blackburn na Stoke kama mbadala wa Sergio Busquets, na inaweza kuwa hivyo kwamba bado inavutiwa naye na angeweza kustawi katika jukumu hilo.

 

Habari Kubwa