Mawazo hupunguza nafasi mwanamke kushika mimba

12Jan 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mawazo hupunguza nafasi mwanamke kushika mimba

UTAFITI mpya unaelekea kuthibitisha kuwa mawazo hupunguza nafasi ya mwanamke kupata mimba, hasa mawazo yanayokuja kipindi cha yai kuingia kwenye mji wa mimba.

"Kama unajiona u mwenye mawazo zaidi kuliko kzawaida yako (kipindi cha yai kuingia kwenye mji wa mimba), una upungufu wa asilimia 40 kuweza kuwa mjamzito katika mwezi huo," anasema muandishi wa utafiti Kira Taylor.

Yeye ni profesa msaidizi wa kitengo cha magonjwa ambukizi na afya ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Louisville kitengo cha Afya ya Jamii na Taarifa za Kisayansi.

Taylor anaamini utafiti wa timu yake ni wa kwanza kuangalia mawazo anayokuwa nayo mwanake katika nyakati mbalimbali katika siku za mwanamke katika mzunguko wa hedhi, kufahamu kama kuna madhara mbalimbali katika hatua mbalimbali.

Katika utafiti huo, watafiti walichambua wanawake 400, wenye umri wa miaka 40 kwenda chini. Wote walikua wakifanya mapenzi na bila kutumia uzazi wa mpango.

"Ni kama theluthi moja tu waliokuwa wakifanya jitihada za kushika mimba, lakini wote hawakuwa wanatumia kondom, na bila njia za kudhibiti utungaji mimba," Taylor anasema.

Kila siku, wanawake hawa walirekodi kiwango chao cha mawazo, kuanzia moja (chini zaidi) mpaka nne (juu zaidi).

Walifanya hivyo kwa mpaka mizunguko 20, au mpaka waliposhika mimba. Kwa wastani, wanawake hao walirekodi hali ya kuwa na mawazo kwa mizunguko nane.

Katika kipindi cha utafiti, wanawake 139 walishika uja uzito. Palikuwa na kupungua kwa asilimia 46 kwa utungwaji mimba kwak ila alama moja ya ongezeko la kiwango cha mawazo wakati wa yai kukutana na mbegu za kiume, watafiti waligundua.

Siku ya 14 ya mzunguko ilikadiriwa kuwa siku ya utungaji mimba.

Athari katika utungaji mimba ziliendelea kuwa sawa hata watafiti walipoingiza vigezo vingine, kama umri, ukubwa wa mwili (kwa kulinganisha urefu mara uzito), utumiaji wa pombe na mara ngapi tendo la ndoa lilifanyika.

Wakati utafiti uligundua uhusiano kati ya mgandamizo wa mawazo na utungaji mimba, haukutthibitisha chanzo na athari.

Katika ugunduzi mwingine unafafanua: "wanawake ambao walishika mimba, walikuwa na kiwango cha juu (cha mgandamizo wa mawazo) kuelekea mwisho wa mzunguko wa hedhi."

Taylor alisema pengine kutokana na kiwango cha homoni, ongezeko la 'estrogen' na 'progesterone' likisababisha wawe na hasira wakati huo.

Dk. Tomer Singer, mkurugenzi wa kitengo cha uzazi katika Hospitali ya Lenox Hill ya jijini New York, alisema utafiti mpya huo umejikita katika wakati ambao unaathiriwa zaidi na mgandamizo wa mawazo.

"Walimudu kutoa mwanga katika wakati muhimu wa kutokuwa na mawazo, na hii ni nusu ya kwanza(ya mzunguko)," alisema.

Timu ya Taylor haikuchunguza ni kwa nini mgandamizo wa mawazo huathiri utungaji mimba wakati yai likiwa limeiva. Lakini, anahisi kwamba "mawazo huharibu mawasiliano ya ishara baina ya ubongo na ovari, na kupunguza nafasi ya yai kuiva."
Singer anakualiana naye.

Alisema wakativ mwanamke anapokuwa na mawazo mengi, homoni zinazohusika na upevushaji yai zinaweza kutibuliwa.
Utibuaji huu wa kawaida unaweza kuzuia mchakato, Taylor alisema, hivyo "inaweza kuwa njia ya asili ya mwili kusema 'Usizae mtot kwa sasa."

Singer alishauri kuwa wanawake wanaweza kupunguza viwango vyao vya mawazo kwa kufanya mazoezi au kutuliza akili yao katika kufikiria jambo fulani tu, miongoni mwa njia nyingine.

Mazoezi mepesi, mara tano kwa juma kwa dakika 30, kunaweza pia kupunguza mawazo, Taylor alisema.

Lakini kufanya mazoezi kupitiliza kunaweza kupunguza uwezekano wa kutungwa mimba, alisema.
Utafiti huo ulichapishwa kwenye mtandao wa kompyuta wa jarida la Annals of Epidemiology.

Habari Kubwa