Zitto akamatwa na polisi, anyimwa dhamana

23Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Zitto akamatwa na polisi, anyimwa dhamana

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto Zuberi amechukuliwa maelezo katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro, Polisi wanaituhumu ziara ya chama cha ACT Wazalendo kutembelea madiwani wao katika kata mbalimbali katika mikoa 8 nchini kuwa ni kosa kisheria.

ZITTO KABWE.

Hivyo, ndugu Zitto ametuhumiwa kufanya Unlawful Assembly S. 74 cap 16 ya Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Lakini kosa hilo amefunguliwa peke yake tu.

Baada ya kuandika maelezo akiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula, tokea saa Saa 4:42 usiku wa jana, mpaka saa 5:40 usiku, Jeshi la Polisi wamekataa kumpa DHAMANA kwa maelezo wanasubiri maelekezo toka kwa wakubwa wao. Hivyo ndugu Zitto amewekwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro.

Pia Jeshi la Polisi limekataa kusema kama dhamana ipo wazi ama la, na kama ipo wazi masharti yake ni yapi, na wamekataa pia kusema iwapo leo watampeleka mahakamani kwa mujibu wa sheria au la.

Emmanuel Lazarus MvulaWakili wa ndugu ZittoMorogoroFebruari 23, 2018

Kabla ya kukamatwa Zitto Kabwe aliandika hivi kwenye ukurasa wake wa Facebook

 

Habari Kubwa