Washushwa vyeo kwa madai ya ulevi

03Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Washushwa vyeo kwa madai ya ulevi

MKUU wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, ameagiza waratibu elimu kata wawili wa kata za Njoge na Lenjulu wilayani humo, kushushwa vyeo kwa madai ya ulevi na kutokuwajibika kazini.

Ndejembi alitoa agizo hilo wakati alipozungumza na waratibu elimu kata, wilayani hapo katika kikao cha kujiandaa  kupokeo wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza mwaka 2018.

 “Hawa watu hawatambui umuhimu wa kazi zao, hivyo naagiza ofisa elimu msingi na sekondari kuwachukulia hatua au muwatafutie kazi nyingine za kufanya na nafasi zao zichukuliwe na watu wengine, ili kuziba nafasi zao haraka," alisema Ndejembi.

Aliwataja waratibu elimu hao wanaotakiwa kuondolewa katika nafasi zao kuwa ni Emmanuel Chiluluse wa kata ya Lenjulu na Venance Mwangasa wa kata ya Njoge.

 

Habari Kubwa