Utoro wanafunzi wasababisha ufaulu kushuka kwa asilimia 20

21Apr 2017
Steven William
Nipashe
Utoro wanafunzi wasababisha ufaulu kushuka kwa asilimia 20

KIWANGO cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi Wilayani Muheza mkoani Tanga kimeshuka kwa asilimia 20 katika kipindi cha mwaka 2016.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Luiza Mlelwa amesema kuwa kushuka huko kumetokana na kukithiri kwa tatizo la utoro kwa wanafunzi, kukosekana chakula mashuleni na mazingira magumu ya kufundishia kwa walimu.

Mlelwa ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha mpango mkakati wa kuboresha Taaluma ya elimu wilayani Muheza kwa mwaka 2017, alisema kutokana na hali hiyo kuna haja kwa wadau wote kupanga mikakati ya kuboresha elimu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Tumbo alisema kuboresha elimu sio suala la wazazi ama wanafunzi pekee bali ni jukum la kila mwananchi ili kuweza kufikia kiwango cha asilimia 100.

Tumbo alisema kuwa mikakati ya kuinua elimu katika wilaya ya Muheza itaanzia katika shule za chekechea, msingi, sekondari na kuendelea ili kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri kupandisha elimu katika wilaya ya
Muheza.

Habari Kubwa