Ushirikina watikisa kesi za Takukuru

21Apr 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ushirikina watikisa kesi za Takukuru
  • *Chui, siafu watumika kushambulia watoa ushahidi

USHAHIDI kwenye kesi zinazosimamiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) unakwama kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ushirikina.

Mkuu wa Sheria na Mashtaka Takukuru Mkoa wa Arusha, Adam Kilongozi, alisema hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kuanzia Julai 2016 hadi Machi mwaka huu.

Alisema baadhi ya kesi zinazosimamiwa na Takukuru zimekuwa zikigubikwa na masuala ya ushirikina na kutolea mfano kesi iliyokuwa ikimkabili Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Prof. Johanes Monyo.

Kilongozi alisema wakati kesi hiyo ikiendelea mashahidi, waendesha mashtaka na hakimu walijawa na hofu kubwa baada ya kutokea kisa cha shahidi mmoja kuvamiwa na chui nyumbani kwake siku aliyotakiwa kufika mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi.

Aliongeza kuwa shahidi mwingine alivamiwa na siafu na kuanza kumshambulia hatua iliyomfanya hakimu aliyekuwa akisiliza kesi hiyo kutaka kuacha kuendelea na shauri hilo baada ya kukuta unga mweusi ndani ya jalada la kesi hiyo.

Habari Kubwa