Ugonjwa huu tishio Shinyanga

17Jul 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Ugonjwa huu tishio Shinyanga

Takwimu za watu wanaougua ugonjwa wa malaria katika Mkoa wa Shinyanga ni kubwa kwa mujibu wa taarifa za mbio za mwenge.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Tellack.

Akitoa taarifa ya mkoa huo, wakati wa kukabidhi mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Tellack amesema katika mikesha ya mbio za mwenge wa uhuru katika mkoa huo jumla ya watu 426 walipima ugonjwa wa maralia ambapo kati ya hao watu 309 waligundulika kuumwa.

Tellack alisema idadi hiyo ya wagonjwa wa maralia ni kubwa na hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kutokomeza maralia hadi kufikia asilimia 0.

Habari Kubwa