TTCL yatakiwa kutambua majukumu yake

22Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TTCL yatakiwa kutambua majukumu yake

Serikali imeitaka kampuni ya simu Tanzania-TTCL kutambua majukumu yake mapya ambayo inatakiwa kuyatekeleza kupitia sheria mpya ya kuanzishwa shirika hilo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashata Nditie.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashata Nditie amesema hayo wakati akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya TTCL jijini Dar es Salaam.

Amesema baadhi ya majukumu ya mawasiliano nchini ni lazima yafanywe na taasisi hiyo Pekee kutokana na unyeti wake hivyo ni Bora wakahakikisha wanakuwa na Huduma Bora zaidi kuliko makampuni mengine.

Naye afisa mtendaji mkuu wa TTCL Waziri Kindamba amesema katika kipindi cha miezi mitatu TTCL imeweza kukusanya madeni yenye thamani ya shilingi Bilioni 6.8 kutoka Kwa wadeni wake na itasitisha Huduma kwa watu ama makampuni au taasisi ambazo wanazidai.

Wiki iliyopita Bunge lilifanya marekebisho ya sheria na kuunda shirika la mawasiliano Tanzania badala ya TTCL, ambapo sasa kinachosubiriwa ni saini ya Rais ili TTCL iwe shirika la Mawasiliano Tanzania.

Habari Kubwa