TBA yaziba 'Expansion Joint' mabweni UDSM 

13Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
TBA yaziba 'Expansion Joint' mabweni UDSM 

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wameanza kurekebisha 'expansion Joint' zilizojitokeza katika mabweni ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Sehemu ya mabwemi mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iliyokuwa inaonesha ina nyufa.

Akizungumza na Nipashe, Mtendaji Mkuu wa TBA, Mhandisi Elius Mwakalinga amesema wameanza kazi ya kurekebisha sehemu hizo siku nyingi na kwamba majengo hayo hayakuwa na nyufa kama waananchi wanavyodai.

Amesema wameanza kuchapia udongo katika maeneo yaliyoonekana yanakasoro, na kwamba walipofanya upimaji katika majengo hayo walikuta matofari na nguzo ziko sawa na hayajapasuka.

Hali ya taharuki ilizuka katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa mwezi huu, baada ya picha zilizokuwa zinaonyesha baadhi ya mabweni mapya ya UDSM yaliyozinduliwa na Rais John Magufuli Aprili 15, mwaka huu yameanza kupasuka.

Habari Kubwa