Soko la tumbaku lashuka

17Jul 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Soko la tumbaku lashuka

Imeelezwa tangu Tanzania ilipojitoa rasmi katika Jumuiya za Nchi Wafanyabiashara Kusini mwa Bara la Afrika (COMMESA) soko la zao la tumbaku limeyumba mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ununuzi wa zao hilo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/18, Kaimu Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika wa wakulima wa Tumbaku Songea, Yasini Makunguru, ameeleza kuwa hali hiyo ya kushuka kwa zao hilo ni kutokana na wanunuzi wa zao hilo kuamua kujitoa na kusababisha kushuka kwa uzalishaji wa zao hilo.

Amesema sababu nyingine ni pamoja na ubadhirifu wa mali za ushirika kunakofanywa na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika na chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Tumbaku cha Songea na namtumbo (SONAMCU).

Katika hatua nyingine baadhi ya wakulima wa zao hilo wilayani Namtumbo wameipongeza serikali kwa dhamira ya kufufua kiwanda cha usindikaji wa zao hilo kilichopo mjini Songea na kuongeza kuwa mpango huo utasaidia kuongeza thamani ya zao hilo na kuongeza ajira kwa vijana.

Habari Kubwa