Simiyu waonywa vitendo vya uvunjifu wa amani

16Apr 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Simiyu waonywa vitendo vya uvunjifu wa amani

JESHI la Polisi mkoani Simiyu, limewataka wananchi mkoani humo kujiepusha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani hasa katika kipindi cha Sikukuu ya Pasaka.

Boneventure Mushongi,

Onyo hilo lilitolewa jana na Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi, Boneventure Mushongi, wakati akiongea na waandishi wa habari.

Kamanda Mushongi, alisema jeshi hilo limeimarisha ulinzi ili kuhakikisha wakristo wa madhehebu yote wanaoadhimisha ibada ya misa za Pasaka wanakuwa salama.

Aliwataka wananchi Simiyu kutoa ushirikiano kwa askari wanaofanya doria kwa kutoa taarifa sahihi juu ya uwapo wa viashiria vya vitendo vya uvunjifu wa amani na kuepuka ulevi wa kupindukia na mikusanyiko isiyo ya lazima.

Aidha, aliwaonya waendesha pikipiki maarufu, bodaboda kuacha kuendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa na kuwataka kuvaa kofia ngumu wao na abiria wao wakati wote wanaposafiri.

Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bariadi, wamelipongeza jeshi hilo kwa kuimarisha ulinzi kupitia doria zinazofanywa mara mara hasa wakati wa usiku kwa kuwa zimesaidia kupunguza uhalifu mkoani hapa.

Habari Kubwa