Shein ataka vijana kujibu 'mapigo' mitandaoni

12Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Shein ataka vijana kujibu 'mapigo' mitandaoni

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka vijana wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mstari wa mbele kukisemea Chama chao hasa pale kinaposemwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii.

Shein ametoa rai hiyo wakati akifungua Mkutano mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), uliofanyika mjini Dodoma, na kuwataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa kujibu hoja. Pia aliwataka viongozi wa UVCCM kuondoa makundi yaliyokuwepo ndani ya umoja huo ili chama kiwe na muonekano mpya katika uwajibikaji.

"Vijana mnatakiwa kuwa mstari wa mbele kukisemea chama vizuri hasa pale kinaposemwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii, ni vyema mkatumia mitandao hiyo kwa kujibu hoja," amesema Dk. Shein.

Katika mkutano huo, UVCCM walifanya uchaguzi wa kuwapa viongozi wapya ambapo Mwenyekiti mpya aliyechaguliwa alikuwa ni Kheri James  ambaye alishinda kwa kura 319 kati ya kura 576 na Makamu Mwenyekiti Thabia Mwita ambaye alishinda kwa kura 286 kati ya 565.

Habari Kubwa