Nyalandu akabidhiwa kadi ya Chadema, avaa gwanda rasmi

19Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Nyalandu akabidhiwa kadi ya Chadema, avaa gwanda rasmi

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho, aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu jijini Mwanza leo Novemba 19,2017 uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu ambako kulikuwa na mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wa nafasi hiyo Godfrey Misana.

lazaro Nyalandu

"Nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya kupigania mageuzi ya kisiasa na ya kiuchumi Tanzania," amesema Nyalandu baada ya kukabidhiwa kadi.

Amesema ana shauku, furaha na heshima kukaribishwa rasmi kuwa mwanachama wa Chadema.

Nyalandu ameongeza kuwa katika majira na nyakati ambazo Taifa linapitia, mabadiliko ya kisiasa nchini
Tanzania ni lazima.

"Naungana na chama hiki pendwa ili tutembee pamoja mtaa kwa mtaa kijiji kwa kijiji tuwaambie
wananchi wakati wa ukombozi ni sasa," alisema Nyalandu.

"Saa ya mabadiliko imefika kwa mtu yeyote miongoni mwetu, tumepewa utayari wa kubadilisha mwelekeo wa nchi," amesema.

Habari Kubwa