Mwandishi wa gazeti la Uhuru apata ajali mbaya

23Feb 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mwandishi wa gazeti la Uhuru apata ajali mbaya

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Uhuru, Mariam Mziwanda, jana usiku Februari 22,2018 amejeruhiwa baada ya kupata ajali iliyohusisha magari matatu, eneo la Tabata TOT jijini Dar es Salaam.

gari la mariam mziwanda likiwa limebanwa na lori baada ya ajali hiyo.

Mziwanda alikuwa akiendesha gari dogo lenye namba za usajili T222 DJX ndipo lilipo gongana na lori la mizigo lenye namba za usajili T 495 na kisha kuingia katikati na kubanwa na lori lingine la mafuta lenye namba za usajili T 748 BMT.

Inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa lori la mzigo ambalo liliacha njia na kupita katika kingo za katikati ya barabara, kisha kupinduka na kuangukia lori la mafuta huku gari lililokuwa likiendeshwa na Mziwanda likiwa katikati.

Baada ya ajali hiyo alikimbizwa katika hospitali ya Muhimbili na baada ya kupimwa kwa kupigwa picha ya C-Ray imebainika hajapata madhara makubwa.

Habari Kubwa