Mwalimu mmoja wanafunzi 236

17Jul 2017
Paul Mabeja
Nipashe
Mwalimu mmoja wanafunzi 236

Shule ya Msingi Mbalawala iliyopo Manispaa ya Dodoma inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa walimu kiasi kwamba mwalimu mmoja hufundisha wanafunzi 236, hali inayofanya kutumia mwezi mmoja kusahisha madaftari yao.

Hayo yamesemwa na mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Moses Risasi wakati wa mkutano wa wazazi uliohudhuriwa na Afisa Elimu wa Manispaa ya Dodoma ambaye aliwatambulisha walimu wapya 10 kwa ajili ya kutatua changamoto ya shule hiyo.

Risasi amesema kuongezeka kwa walimu hao kutasaidia kuongeza ufanisi katika kazi zao kutokana na kuelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi. Shule ilikuwa na walimu saba wanaohudumia wanafunzi 922.

“Kama mwalimu wangu wa darasa la pili alikuwa anafundisha wanafunzi 236, hivyo utaona ni jinsi alikuwa anapata shida unakuta muda mwingine hasahihishi madaftari hata mwezi mzima,” alisema Risasi.

Habari Kubwa