Mrembo jambazi anaswa, auawa kwa risasi

14May 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Mrembo jambazi anaswa, auawa kwa risasi

MWANAMKE aliyekuwa akidhaniwa kwamba ndiye jambazi mrembo kuliko wote katika jiji la Nairobi, Kenya, aliuawa baada ya majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Kayole, mchana wa jua kali katikati ya wiki.

Ilidaiwa kabla ya kuuawa, mrembo huyo alikuwa na majambazi wenzake watatu wa kiume waliokuwa wakiwapora mali wakazi wa eneo hilo.
Awali, Polisi walijulishwa na raia wema kuhusiana na mahala walipokuwa majambazi hao kabla ya kuwavamia, wakiwataka kujisalimisha.

Badala yake, majambazi hao waliwarushia risasi risasi polisi, ambao nao walilazimika kujibu mapigo, hivyo kuwauwa watuhumiwa wawili waliokuwa wakijaribu kukimbia.

Bastola iliokotwa katika eneo la tukio, ikiwa na risasi sita za mduara wa milimita 9 kila moja na miili ya wafu ilibebwa na kupelekwa katika mochwari ya jiji la Nairobi kwa uchunguzi zaidi.Ilielezwa kuwa kundi hilo hatari la majambazi halikuwa likifahamika kwa urahisi na kwamba polisi walijulishwa kupitia kundi mojawapo la kuchati la mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kayole, Joseph Gichangi, polisi walikuwa bado wakiwatafuta majambazi wengine wawili waliofanikiwa kukimbia na kwamba, mrembo jambazi ambaye hakumtaja jina, alikuwa ni mke wa mmoja wa watuhumiwa hao.

Ilidaiwa violevile kuwa mrembo huyo jambazi alishitukiwa na mmoja wa watumiaji wa mtandao wa kijamii, jina limehifadhiwa, kama mke wa mmoja wa majamabzi hatari katika eneo la Kayole.
(The Standard)

Habari Kubwa