Mbowe asisitiza ushirikiano wabunge mambo yenye maslahi kwa taifa

21Apr 2017
Thobias Mwanakatwe
Nipashe
Mbowe asisitiza ushirikiano wabunge mambo yenye maslahi kwa taifa

KIONGOZI wa Kambi rasmi Bungeni, Freeman Mbowe, ametaka wabunge kuwa na urafiki ambao utakuwa na taswira chanya kwa maslahi ya Taifa letu.

Freeman Mbowe.

Amesema hayo leo alipokuwa akitoa salamu za rambi rambi wakati wabunge wakiaga mwili wa mbunge wa viti maalum (Chadema), Dk. Elly Macha, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma aliyefariki Machi 31, nchini Uingereza.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, alisema ushirikiano ulioonyeshwa na serikali na Bunge kwa ujumla tangu marehem alipougua hadi mauti yanamkuta ni umejenga urafiki mzuri na wa kuigwa katika mambo ya msingi.

Alisema ushirikiano huo umejenga taswira nzuri kwa wabunge na kujifunza kwamba urafiki wa aina hiyo unaweza kujengwa hata katika kusimamia mambo ya msingi yenye maslahi kwa Taifa.

Naye Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema serikali imepata mshtuko kutokana na kifo cha mbunge huyo na kwamba wabunge waige mambo mazuri yaliyokuwa yakifanywa na mbunge huyo.

Wabunge na mawaziri wakiongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Waziri Mkuu Majaliwa wamejumuika kuuaga mwili wa Dk. Macha ambao utasafirisha kwenda mkoani Kilimanjaro kwa maziko.

Habari Kubwa