Mapya yaibuka uspika EALA

27Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mapya yaibuka uspika EALA

Shirika la Marafiki wa Afrika Mashariki (FEA), limeingilia kati mvutano wa uchaguzi wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), baada ya wabunge wa Tanzania na Burundi kutangaza kutotambua ushindi wa Martin Ngoga.

Wabunge kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini, walifanya uchaguzi wa spika baada ya vuta ni kuvute iliyosababisha wabunge kutoka Tanzania na Burundi kususia uchaguzi huo uliofanyika Desemba 19, mwaka huu.

Akizungumzia sintofahamu hiyo, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa FEA, lenye makao yake jijini hapa, Moses Allan Adam, amewalaumu wabunge wa Bunge la nne la Afrika Mashariki kwa ubinafsi dhidi ya wananchi wanaounda jumuiya hiyo.

Amesema hali hiyo imesababisha  shughuli za jumuiya hiyo kwenda mrama na kupoteza mwelekeo wa maslahi ya   pamoja ya wananchi wa Afrika Mashariki.

Habari Kubwa