Ipp media yang'ara tuzo za uandishi mahiri

21Apr 2017
Beatrice Shayo
Nipashe
Ipp media yang'ara tuzo za uandishi mahiri

WAANDISHI wa Habari 12 kutoka Kampuni ya IPP Media wameteuliwa kushiriki kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT).

baadhi ya waandishi wa habari.

Waandishi hao ni Salome Kitomari, Gwamaka Alipipi, Neema Emmanuel, Abdul Mitumba, Sanula Athanas, Abdul Kingo, Lasteck Alfred na Mwidini Msamba wote wanatokea gazeti la Nipashe.

Wengine ni Gerald Kitabu, Lusekelo Philemon, Henry Mwangonde ambao ni waandishi wa Guardian na Frank Mshana wa ITV.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tuzo za EJAT, Kajubi Mukajanga, alisema kuwa jumla ya waandishi wa habari 66 wameteuliwa kuwania tuzo hizo katika madaraja 19.

Habari Kubwa