Gambo: Mnaotaka kutoa rambirambi mfuate utaratibu

19May 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Gambo: Mnaotaka kutoa rambirambi mfuate utaratibu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wananchi na taasisi zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Kauli hiyo imekuja wakati jeshi la polisi mkoani Arusha likiendelea kuwahoji Meya wa jiji la Arusha Kalst Lazaro na watu wengine wanne kuhusiana na tuhuma za kutengeneza mkusanyiko usio na kibali serikali wakati wa kwenda kutoa rambirambi katika shule hiyo.

Gambo amesema masuala ya fedha yana changamoto na yasiposimamiwa vizuri lengo tarajiwa haliwezi kutimia, na kwamba serikali itaendelea kuwadhibiti wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi.

Habari Kubwa