Diwani wa Chadema, auwawa kwa mapanga

23Feb 2018
Ismael Mohamed
Nipashe
Diwani wa Chadema, auwawa kwa mapanga

Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Namwawala wilaya ya Kilombero Godfrey Luena ameuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake.

Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Namwawala wilaya ya Kilombero Godfrey Luena.

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje- Chadema, John Mrema na kusema ni kweli Diwani wao ameuliwa akiwa nyumbani kwake jana (Alhamisi) Februari 22, 2018.

"Ni taarifa za kweli aliuwawa jana Luena, majira ya saa 1 usiku kwa kukatwa katwa mapanga akiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana. 

Mpaka sasa hatujaelewa chanzo cha kifo chake kwa kuwa kilitokea usiku lakini tumekwisha toa taarifa kwa Jeshi la Polisi na walienda eneo la tukio wakasema watafuatilia", amesema Mrema.

Kwa upande mwingine, Mrema amesema kama chama bado wanafuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili waweze kubaini chanzo cha tukio hilo ni nini pamoja na aliyehusika na mauaji hayo.

 

Habari Kubwa