TPSF yafungua ofisi Guangzhou

08Jan 2017
Christina Mwakangale
Nipashe Jumapili
TPSF yafungua ofisi Guangzhou

TAASISI ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), imefungua ofisi nchini China, ili kupanua wigo na fursa za kibiashara, uwekezaji na kukuza uchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema ofisi hiyo iliyoko mjini Guangzhou katika mkutano ulioitishwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni jijini aliwaeleza nia ya serikali ya kushirikiana na sekta binafsi hususan katika kukuza wigo wa kibiashara na uwekezaji.
Alisema ofisi hiyo itatoa fursa ya ajira kwa Watanzania waishio China na pia kwa kipindi cha miaka mitatu haitalipiwa kodi ya pango.

“Makamu wa Rais tumekutana naye wiki hii, akitueleza alivyofanikisha kupatikana kwa ofisi nchini China ili kufanikisha kukuza mawasiliano ya karibu zaidi kutoa fursa ya kibiashara na uwekezaji,” alisema Simbeye.

Alisema ipo haja ya serikali kuendelea kukuza na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini, hususan katika sekta ya viwanda na biashara.

Habari Kubwa