Mbunge Moro akabidhi mil. 20/- mshindi Biko

16Jul 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Mbunge Moro akabidhi mil. 20/- mshindi Biko

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood, jana alimkabidhi mshindi wa Sh. milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko, Elizabeth Damian, ambaye aliibuka kinara katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo (Ijue Nguvu ya Buku) iliyofanyika Jumatano, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Abood alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri fedha zake ili ziweze kumnufaisha kiuchumi.

Alisema jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa, ni sehemu muwafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, na hivyo wananchi wake wa Morogoro na Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.

“Wakati nawapongeza Biko kwa kubuni michezo hii inayotoa mamilioni kwenu washindi, lakini pia nakupongeza wewe mwananchi wangu wa Morogoro kwa kuwa kati ya wachezaji wenye bahati kubwa kiasi cha leo kukabidhiwa Sh. milioni 20,” alisema.

Akizungumzia ushindi wake, Elizabeth aliyekabidhiwa fedha zake benki mjini Morogoro, alisema hakuamini kama angeweza kuibuka na ushindi huo mnono, jambo linalomfanya kuwa na furaha isiyoelezeka.

Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kuacha kucheza Biko ni kukubali kukosa fursa za kiuchumi ambazo kila mtu anaweza kuzipata kwa kucheza mara nyingi bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wa Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel kwa kufanya miamala kwenye simu zao kuanzia Sh. 1,000 na kuendelea.

“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu tiketi moja ya Sh 1000 inapofanywa kwa njia ya muamala kwenye simu husika, itampatia nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh. 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh. Milioni moja, pamoja na donge nono la Sh milioni 20 zinazopatikana kila Jumatano na Jumapili, huku namba ya kampuni yetu ikiwa ni 505050 na kumbukumbu namba ni 2456.

“Kila mtu anaweza kushinda zawadi nono kutoka Biko, hivyo unachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi kama njia ya kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi mnono kutoka kwenye bahati nasibu yetu ya Biko,” Alisema Heaven.

Tangu kuanza kwa bahati nasibu ya Biko nchini Tanzania ikiwa ni miezi miwili tu, tayari imeshatoa zaidi ya Sh. bilioni moja kwa washindi wake katika kipindi cha Mei na Juni, ikiwa ni ishara kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakiitumia fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko.

Habari Kubwa