NMB yanogesha mashindano ya SHIMIWI

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:13 PM Sep 27 2024
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Dotto Biteko akifurahia jambo na Naibu Waziri wa Michezo, Utamaduni na Sanaa, Hamis Mwinjuma na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima wakati wa uzinduzi wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya SHIMIWI.
Picha:Mpigapicha Wetu

Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) imefunguliwa rasmi kuzikutanisha timu zinazowajumuisha watumishi wa serikali kutoka kwenye wizara, taasisi, wakala za serikali, ofisi za wakuu wa mikoa, halmashauri, pamoja na manispaa.

Uzinduzi huu umefanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Dotto Biteko aliyeambatana na Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma pamoja Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima.

Uwakilishi wa benki umeongozwa na Meneja wetu Mwandamizi wa Mahusiano ya Benki na Serikali, Josephine Kulwa, Meneja Mwandamizi Huduma za Kibenki kwa Serikali, Amanda Feruzi, pamoja na wafanyakazi wengine.