Koka: Kuwachagua viongozi wa CCM kutarahisisha maendeleo Kibaha

By Julieth Mkireri , Nipashe
Published at 04:48 PM Nov 23 2024
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka
Picha:Mpigapicha Wetu
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema endapo wananchi watachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) itarahisisha kupambana na kutekeleza mipango ya maendeleo kwa pamoja.

Amesema tayari kuna maendeleo yamefanyika katika mji wa Kibaha ambayo yameatokana na kuwa na Viongozi wa chama kimoja ambao wameshirikiana kwa kila hatua.

Koka ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kampuni za chama cha mapinduzi (CCM) Kata ya Kongowe zilizofanyika katika eneo la Bamba na kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi wengine.

Koka amesema kwamba wakichaguliwa viongozi wote wa CCM inatoa urahisi wa ushirikiano katika utekelezaji wa miradi mbalimbali na kupanga mambo ya maendeleo kwa pamoja tofauti na kuchanganya na vyama vingine.

1

Amesema kwamba kwa sasa Jimbo la Kibaha Mjini limekuwa na mabadiliko ya kimaendeleo ambayo yameatokana naa juhudi zake kwa kushirikiana na wenyeviti ambao wamemaliza muda wao na endapo watachaguliwa tena itakuwa rahisi kwake kushirikiana kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Diwani wa Kongowe Hamis Shomari amesema kwamba wagombea ambao wameteuliwa na chama hicho endapo watachaguliwa na wananchi watashirikiana kuondoa vikwazo maeneo yenye tatizo.

Shomari amewaomba wananchi kuchagua wagombea wa Chama hicho ambao kwa pamoja watashirikiana kuleta maendeleo katika kata hiyo na kutekeleza miradi ambayo imeanzishwa.

Nuru Awadh ambaye ni mgombea mtaa wa Miembe Saba B amesema endapo atachaguliwa atashirikiana na wananchi kujenga Zahanati pamoja na kusimamia ukarabati wa barabara iweze kupitika muda wote.
2