PSSSF mshindi wa kwanza tuzo za NBAA uandaaji bora wa mahesabu, 2023

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:15 AM Nov 30 2024
PSSSF mshindi wa kwanza tuzo za NBAA uandaaji bora wa mahesabu, 2023.
Picha:Mpigapicha Wetu
PSSSF mshindi wa kwanza tuzo za NBAA uandaaji bora wa mahesabu, 2023.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza ya umahiri katika uaandaji wa taarifa za mahesabu kwa mwaka unaoishia 2023, katika kundi la hifadhi ya jamii.

Tuzo hiyo imepokelewa na Meneja wa Fedha, PSSSF, Vonness Koka, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, katika hafla ya utoaji tuzo ulioratibiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Wizara ya Fedha, Benjamin Mashauri.

“Tunamshukuru Mungu kwa kupewa hii tuzo, tunapokea tuzo hii kwa mara ya tatu mfululizo, pongezi kwa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko, Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti yake na watumishi wote wa PSSSF kwa ujumla; Hususani kurugenzi ya fedha kwa kuwezesha kupatikana kwa tuzo hii. Tuzo hii iwe chachu ya kuhakikisha kwamba mahesabu yetu yanaandaliwa vyema kila wakati”. alisema Koka.