MAJAJI na Mahakimu zaidi ya 392 wanatarajia kushiriki katika kongamano na mkutano mkuu wa 21 wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Afrika Mashari (EAMJA),utakaofanyia jijini Arusha kuanzia Disemba 2 hadi 7 mwaka huu.
Aidha ufunguzi wa mkutano huo wa EAMJA utafunguliwa Disemba 3 mwaka huu na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye atakuwa mgeni rasmi siku hiyo.
Hayo yalisemwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani,Dk.Gerald Ndika,ambaye ni Mwenyekiti wa maandalizi ya kongamano na mkutano huo,wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa.
Jaji Ndika, alisema chama hicho,kilianzishwa mwaka 2000 na kuzinduliwa nchini Uganda mwaka 2001 na hadi sasa kimetimiza miaka 2024 tangu kuanzishwa kwake.
Alisema lengo la chama hicho,ni kutoa jukwaa kwa wahusika kukutana na kujadiliana namna bora ya kuboresha utendaji kazi wao,kupeana uzoefu na kujadiliana kuhusiana na changamoto na mafanikio yaliyopata.
Pia alisema lengo linguine la chama ni kutetea na kulinda uhuru wa Mahakama kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na utawala bora wa sheria.
“Nchi yoyote ile haiwezi kuwa na maendeleo bora ikiwa na changamoto za utawala wa sheria na mfumo wa utoaji wa haki, hivyo jukwaa hili linawawezesha Majaji na Mahakimu kukutana na kubadilishana uzoefu,”alisema Jaji Ndika.
Vilevile alitaja maji ya nchi ambazo washiriki wanatokea kuwa ni Tanzania Bara,Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi,Sudani ya Kusini na Zanzibari huku nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) na Somalia bado hawajathibisha wawakilishi wao kuudhuria katika mkutano huo.
“Maudhui ya mkutano tutaangalia uboreshaji wa mifumo ya utoaji haki kwa ajili ya kuimarisha utangamano na ukuzaji uchumi katika ukanda wa EAC,pia tutaangalia uboreshaji wa mifumo ya utoaji haki,”alisema.
Pia alisema katika kongamano na mkutano huo,utawawezesha kujadiliana na kupitia maeneo mengine mahususi matano ambayo ni kuangalia utendaji kazi katika eneo la utoaji haki kwa haraka zaidi.
Alisema eneo lingine, litakuwa kuangalia progamu za maboresho ya mifumo ya utoaji haki jinai,programu za maboresho ya mfumo wa utoaji haki katika mashauri ya madai,uboreshaji utoaji haki kwenye migogoro ya kazi,Matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na uimarishaji wa utoaji wa maamuzi kuhusiana na mashauri ya makosa ya jianai na uhamishaji wa fedha unaovuka mipaka.
Naye Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu wa Mahakama Tanzania (JMAT), John Kahyoza,alisema watahakikisha wanawajengea uwezo Majaji na Mahakimu ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Alisema watahakikisha wahusika wanashiriki kwenye mikutano hiyo kwa ajili ya kuwapatia elimu na ujuzi wa mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya mipaka ya Tanzania na nje ya miapaka ya nchi.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED