Ben Pol aachia 'mpini' mpya

Akizungumza na gazeti hili, Pol alisema wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One Love Records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter.

Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoka na huo wa 'Phone'.

Alisema tayari wimbo huo umeanza kusikika kupitia vituo mbalimbali vya radio, huku ujio wa video yake ukiwa njiani.

"Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu,"alisema Pol.