Banda atoa masharti Simba

Akizungumza na gazeti hili jana, Banda alisema mbali na timu hiyo kutokuwa na uhakika wa kushiriki katika mashindano ya kimataifa mwakani, lakini atakuwa tayari kusaini mkataba mpya kama atalipwa kutokana na kile alichopendekeza.

Banda alisema pia mchakato wake wa kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini bado haujafa na anaweza kuondoka baada ya msimu huu kumalizika.

"Mkataba mpya nitasaini kama nitapata kile nilichowaambia, tumeshafanya mazungumzo ya awali na wanajua nini ninataka, ikishindikana nitaenda tena Afrika Kusini kujaribu bahati yangu maana wakati ule mkataba ndio ulinikwamisha, klabu zinakwepa kulipa ada ya uhamisho," alisema beki huyo.

Aliongeza kuwa hata hapa nchini klabu mbalimbali zinamfuata, lakini lengo lake ni kuona anasonga mbele.

Banda ni mmoja wa wachezaji wa Simba wanaomaliza mkataba mwishoni mwa mwezi huu baada ya msimu wa ligi kumalizika.