Ugonjwa huu tishio Shinyanga

Akitoa taarifa ya mkoa huo, wakati wa kukabidhi mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Tellack amesema katika mikesha ya mbio za mwenge wa uhuru katika mkoa huo jumla ya watu 426 walipima ugonjwa wa maralia ambapo kati ya hao watu 309 waligundulika kuumwa.

Tellack alisema idadi hiyo ya wagonjwa wa maralia ni kubwa na hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili kutokomeza maralia hadi kufikia asilimia 0.