Manji ajipeleka Kisutu leo

Aprili 18, mwaka huu, Manji hakuwepo mahakamani wakati kesi hiyo ilipotajwa huku upande wa utetezi ukidai kuwa  ni mgonjwa.  

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi Cyprian Mkeha, iliamuru Manji kufika mahakamani kesi yake inapopangwa kutajwa.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Adolf Nkini, ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa ambapo Hakimu Mkeha alisema kesi hiyo itatajwa Juni 23, mwaka huu, na dhamana ya mshtakiwa inaendelea.