Mfanyabiashara awaburuza kortini vigogo

Katika kesi ya madai namba 8 ya 2017, iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupokelewa Ofisi ya Msajili wa mahakama hiyo, Aprili 27, mwaka huu, Mollel anadai walalamikiwa wanashikilia hati yake ya nyumba namba C.T 22906, L.O 253119 ya kiwanja namba 231 eneo ‘DD’ lililopo Mianzini mjini Arusha ambalo amemilikishwa kwa miaka 99.

Alidai kuwa kiasi cha fidia anachodai kinatokana na vigogo hao kushikilia hati ya nyumba yake kwa zaidi ya miaka miwili sasa na hivyo kumfanya ashindwe kuitumia kukopa fedha taasisi za fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara zake.

Alidai awali alikopa kiasi kama hicho na kuweza kurejesha kwa wakati.

Alidai Agosti 22, 2014 mlalamikiwa wa kwanza ambaye ni RCO kupitia afisa wake alikamata cheti cha hati hiyo mbele ya Dani Makanga, Shija Kija, Inspekta Msaidizi Goodluck na Duncan Oola, kufuatia utaratibu wa kukamata mali wa ofisi ya uhalifu.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikizwa Juni 22, mahakamani hapo.