11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Prisons kuongeza wa5 CAF
 
2008-05-11 10:59:03
By Bahati Mollel

Timu ya Prisons imesema itaongeza wachezaji watano ili kujiimarisha kwa michuano ya Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika mapema mwakani.

Kocha mkuu wa Prisons Juma Mwambusi aliliambia Lete RAHA kwa njia ya simu juzi Ijumaa kuwa amefanya tathmini ya ligi ya kuu Bara na ameona mapengo matano.

``Mapengo hayo yapo katika nafasi ya ushambuliaji, kipa, kiungo na ulinzi,`` alisema Mwambusi na kueleza zaidi kuwa ``wachezaji hao wanaweza kuongeza mara tutakapoanza mazoezi baada ya wiki mbili.``

``Siwezi kuibadilisha kwa kiasi kikubwa timu yangu. Ninataka walinzi wawili... hizo nafasi nyingine (mchezaji) mmoja mmoja, na kwa kuwa tutaanza mazoezi mapema sidhani kama watashindwa kuzoeana na wenzao.``

Uongozi wa Jeshi la Magereza linalomiliki timu hiyo umeshaarifiwa, alisema, na kwamba pamoja na usajili, jeshi hilo pia linafanya taratibu za kufanikisha kuanza mapema huko kwa mazoezi na mechi nyingi za kirafiki na klabu za nje ya nchi kama Zambia na Malawi.

Alisema ili timu hiyo iweze kufanya vizuri Afrika uongozi wa klabu hiyo unapaswa ushirikiane na serikali kufanya ukarabati wa Uwanja wa Sokoine katika uzio, vyumba na sehemu ya kuchezea ili waweze kuutumia kwenye mechi za klabu za Afrika.

``Mechi nyingi za kimataifa zimekuwa zikifanyika Uwanja wa Taifa.

Sasa huko wamezoea timu za Simba na Yanga hivyo nadhani hatutapata washangiliaji wengi kama ambao tutapata tukichezea kule Sokoine,`` alisema Mwambusi.

Kwasasa kocha huyo anaifundisha timu ya mkoa wa Mbeya itakayoshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Taifa yaliyopangwa kuanza keshokutwa, Jumanne jijini.

Akizungumzia siri ya Prisons kutwaa nafasi ya pili, alisema inatokana na nidhamu kubwa aliyojenga kwa wachezaji wake, na ndoto ya kutwaa ubingwa ingawa bahati haikuwa yao.

Prisons iliwahi kicheza michuano ya klabu ya Afrika mwaka 1999 na 2004.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.