11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Sportsnews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Coastal walaumu wakazi Tanga
 
2008-05-11 10:56:23
By Mwandishi Wetu

Kushuka daraja kwa mabingwa wa zamani na timu iliyoanza kwa kishindo ligi kuu ya Bara msimu huu kwa kuvifunga mfululizo vigogo vya soka Simba na Yanga, timu ya Coastal Union imelalamikia kutopewa ushirikiano wa kifedha na wananchi na makampuni ya mkoani Tanga.

Katibu mkuu wa Coastal Union Salim Bawazir alisema endapo timu hiyo ingepata misaada ya kifedha kwa ajili ya kulipa posho na mishahara ya wachezaji, isingeshuka kwenye ligi kuu.

Mishahara na posho vingewafanya wachezaji wacheze kwa ari na moyo, alisema Bawazir ambaye timu yake iliundwa na wachezaji wengi chipukizi.

``Sisi ndio tulikuwa timu pekee hapa mkoani, hivyo tulistahili kupewa ushirikiano wa udhamini na watu wetu wa hapa,`` alisema Bawazir kwa simu.

``Lakini hawakufanya hivyo hadi tunashuka. Tunasikitika lakini hatuna jinsi, kazi iliyobaki ni kuipandisha tena daraja.``

Timu hiyo iliyokuwa bingwa wa Bara miaka 20 iliyopita ilianza kudorora baada ya kuingia kwenye mzozo mkali wa posho na wachezaji wake, uongozi ukituhumiwa kutangaza mapato kidogo kuliko kilichokuwa kikipatikana kwenye mechi za nyumbani.
Hali mbaya kifedha pia ilisababisha kukimbiwa na kocha mkuu Rashid Shedu wa Kenya.

Coastal Union iliyokuwa imerudi ligi kuu kwa mara ya kwanza mwaka jana tangu kushuka mwaka 2002, ilimaliza ikiwa na pointi 28 tu. Tatu zikiwa ni za mezani.

Yanga ilitwaa ubingwa kwa kuwa na pointi 49 kutokana na mechi 26.

  • SOURCE: Lete Raha
TODAY
-----------------------------------------------
Editorial
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.