Sportsnews |
 |
NAVIGATION |
 |
|
 |
|
|
 |
SEARCH |
 |
|
|
|
 |
SPECIAL |
|
|
 |
|
|
 |
ARCHIVES |
|
|
 |
|
|
 |
|
 |
|
|
|
Viongozi waporwa timu ya Malindi
2008-05-11 10:55:01
By Bahati Mollel
Wazee wa klabu kongwe ya Malindi ya Zanzibar wamewanyang`anya timu viongozi na kuwakabidhi wanachama kwa ajili ya kuinusuru na janga la kushuka daraja la ligi kuu.
Msemaji wa wanachama hao Ali Said alisema juzi Ijumaa kwa njia ya simu kuwa uongozi huo umekuwa kwenye malumbano ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu na kushindwa kuihudumia timu hiyo iliyokuwa ikikaa nje kidogo ya mji katika eneo la Chukwani.
Said alisema baada ya wanachama kukabidhiwa timu hiyo tayari wameihamisha kutoka Chukwani na kuipeleka kwenye viwanja vya Malindi ambavyo ni karibu na makao makuu ya klabu hiyo.
``Uongozi umekuwa ukilumbana sana hadi kufikia kushindwa kutoa usafiri kwa timu wa kuwapeleka mazoezini na kuwarudisha,`` alisema Said na kueleza zaidi kuwa ``wakati mwingine wachezaji walishindwa kwenda mazoezini.``
Alisema wanachama wamepewa jukumu la kuinusuru na janga la kushuka daraja.
Malindi ambayo iliwahi kuwa timu tishio Zanzibar na kwenye ligi kuu ya Muungano kwa ujumla, inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani katika msimamo wa timu 12 ikiwa na pointi 12 tu, huku zikitakiwa kushuka timu mbili za mwisho.
Said alisema wanachama wa klabu hiyo iliyokuwa tishio katika miaka ya katikati na ya mwishoni ya 1990 wameutaka uongozi mzima wa klabu hiyo kujiuzulu ili kutoa nafasi kwa wenye mapenzi nayo kuiendeleza timu hiyo.
Katika hatua nyingine klabu hiyo imewaongeza kupitia usajili mdogo wachezaji wakongwe Amour Aziz na Waziri Seif ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji.
Pia Said alisema Mweka hazina msaidizi Humud Kao amejiuzulu wadhifa huo kwa madai ya mizozo ndani ya klabu hiyo.
|
|
 |
TODAY |
|
|
----------------------------------------------- |
Editorial |
|
|
----------------------------------------------- |
Business
bits |
|
|
----------------------------------------------- |
|
|
| |
 |
|