|
ZFA wagoma
2008-05-11 10:53:44
By Mwandishi Wetu, Zanzibar
Uongozi wa Chama cha soka cha Zanzibar, ZFA, umeendelea kuigomea serikali kuhama kwenye ofisi zake zilizopo Uwanja wa Amaan ili kupisha ukarabati, na sasa unataka utafutiwe ofisi nyingine.
Msemaji wa ZFA, Maulid Hamad alisema jana Jumamosi kuwa wanaendelea kuisisitizia serikali kuwatafutia ofisi yenye hadhi ya chama hicho ili waweze kuhama baada ya kutakiwa kufanya hivyo mapema mwezi uliopita.
Maulid alisema kutokana na utaratibu wa muda mrefu, serikali tangu zamani imekuwa ikitoa majengo yake na kuvipa vyama vya michezo.
|