17 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wakulima wa kijiji cha Malula wagoma kutoa ardhi yao kwa serikali
 
2008-05-17 15:06:08
Na Radio One Habari

Wakulima wa kijiji cha Malula wilaya ya Arumeru wamegoma kutoa ardhi yao kwa serikali kwa ajili ya kujenga ukanda maalum wa kibishara na uchumi-EPZ wakidai kuwa hawajashirikishwa.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wamesema wameshangazwa na hatua ya serikali kutuma wataalamu wa kupima ardhi yao bila kupata ridhaa yao.

Wamesema uongozi wa kijiji na kata umetumia mihutasari ya kugushi na kisha kupeleka halmashauri ya wilaya hiyo ambayo ilipitisha uamuzi wa eneo hilo kuchukuliwa na wananchi hao kupewa fidia.

Eneo hilo lenye ukubwa wa ekari elfu tano linalozalisha chakula kingi kutokana na kuwa na mvua za uhakika, hutegemewa na wananchi wa Kaskazini mwa nchi kwa chakula.

Akijibu madai ya wakulima hao mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Saiguran Mollel amesema suala hilo limepelekwa kwa mkuu wa mkoa wa Arusha na kwamba wakulima hao wasubiri uamuzi wake kwani walishakata rufaa kwake.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.