17 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Chakula kilichotolewa kwa ajili ya mkoa wa Manyara hazijulikani zilipo
 
2008-05-17 15:01:31
Na Radio One Habari

Zaidi ya tani 500 za chakula cha njaa kilichotolewa kwa ajili ya mkoa wa Manyara hazijulikani zilipo na zinahofiwa kutoroshwa na kuuzwa nchi jirani.

Wakizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo viongozi wa wilaya za mkoa huo wamesema chakula hicho kilichoombwa kwa ajili ya wananchi wanaokabiliwa na njaa katika wilaya zao, kimechukuliwa na baadhi ya watu kwa kutumia vibali vya bandia.

Viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya wamesema, baada ya kuona chakula hakiwafikii walengwa ,walifuatilia na kugundua kuwa kimechukuliwa na na watu waliodai kupewa vibali na halmashauri za wilaya hizo kukisambaza, ingawa hakikufikishwa katika baadhi ya maeneo.

Akizungumzia suala hilo mkuu wa mkoa wa Manyara Bwana Henry Dafa Shekifu amekiri kupokea taarifa hizo na amesema mkoa unafuatilia na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika watakaobainika kushiriki kwa namna yeyote katika njama hizo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.