|
Shule ya sekondari ya Mtunduru iliyopo Singida Vijijini yapatiwa msaada
2008-05-17 15:00:30
Na Radio One Habari
Benki ya CRDB tawi la Singida imetoa msaada wa shilingi milioni-14 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya sekondari ya Mtunduru iliyopo Singida Vijijini.
Meneja wa CRDB tawi la Singida Bwana Philemon Pindapinda amesema benki hiyo pamoja na kufanya biashara imeamua kutoa msaada huo, ili kuitikia wito wa taifa katika kuchangia elimu.
Amesema CRDB tawi la Singida limeshatoa msaada mwingine katika shule ya msingi Kisasida kwa ujenzi wa kisima cha maji na amewataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa kuchangia katika ujenzi wa shule ili watoto waeze kupata elimu iliyobora.
|