16 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha imeshindwa kufikia malengo
 
2008-05-16 15:48:22
Na Radio One Habari

Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha imeshindwa kufikia malengo katika hutoaji wa elimu kwa watoto wote kutokana na wazazi wengi wilayani humo kuwaficha na wakati mwingine kuwaua watoto wenye ulemavu.

Hayo yamebainika wakati wa uzinduzi wa mkakati wa mabadiliko wa kitaifa wa miaka kumi kwa wilaya Ngorongoro unaoratibiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lenye makao makuu yake nchini Uingereza la OXFAM ambao ulianza mwaka jana na unatarajiwa kukamilika mwaka 2017.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Bwana Simon Soinda ameitaka jamii hiyo ambayo sehemu kubwa ni ya wafugaji ibadilike na kukubali watoto wenye ulemavu wapelekwe katika shule maalumu badala ya kuwaficha.

Akizindua mkakati huo , Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bwana Jowika Kasunga amesema maisha ya kuhamahama ya jamii ya wafugaji katika wilaya hiyo bado ni changamoto kubwa kiuchumi kwani utamaduni huo holela unachangia upotevu wa mali na ukosefu wa elimu kwa wototo.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.