|
Tanzania kupata mafanikio iwapo itaimarisha kilimo cha umwagiliaji
2008-05-15 17:36:40
Na Radio One Habari
Tanzania inaweza kupata mafanikio makubwa kupitia sekta ya kilimo, kama itaimarisha kilimo cha umwagiliaji hasa kwenye mikoa inayopitiwa na mito mikubwa na maziwa.
Kaimu Mkuu wa mkoa Iringa Bwana Erasto Mbwilo amesema hayo wakati akizungumza na wadau na wataalam wa kilimo cha umwagiliaji kutoka mikoa sita ya hapa nchini wanaokutana mjini Iringa kujadili mchakato wa kuanzishwa kwa sera ya taifa ya umwagiliaji.
Amesema kuna umuhimu wa kuwaandalia wakulima mazingira yatakayowavutia zaidi kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji, kwa kutengeneza taratibu za kisera na kisheria zitakazolinda matumizi ya rasilimali ya maji na vyanzo vyake visiharibiwe.
Bwana Mbwilo rasilimali za mito, maziwa na mabwawa zilizopo nchini ni fursa kwa wakulima wanaotaka kuingia kwenye kilimo cha umwagiliaji, lakini pia lipo tatizo la sera za nchi kuhusu matumizi ya maji pamoja na zile zinazohusu uhifadhi wa mazingira na vyanzo vya maji.
|