|
Kadhi Mkuu wa Zanzibar afariki dunia
2008-05-13 17:55:52
Na Radio One Habari
Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Ali Hatib Mlanzi amefariki dunia ghafla leo nyumbani kwake Jang`ombe mjini Zanzibar.
Taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi zimesema Sheikh Mlanzi amefariki dunia mapema asubuhi wakati akijiandaa kwenda kazini.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kadhi Mkuu huyo hakuugua na amefariki dunia miaka miwili tangu ashike wadhifa huo.
Aidha taarifa hiyo imesema maziko ya marehemu tayafanyika leo saa kumi jioni katika makaburi ya Shakani wilaya Magharibi Unguja.
|