11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Wanaowafungia watoto walemavu washitakiwe
 
2008-05-11 20:03:26
Na Radio One Habari

Watu wenye ulemavu mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wenye tabia ya kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu kwa kuhofia kuchekwa.

Ushauri huo umetolewa na umoja wa Chama cha Watu wenye Ulemavu-CHAWATA tawi la Sumbawanga wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho mjini Sumbawanga.

Katibu wa chama hicho kitengo cha wanawake Bi. Yasinta Chipeta amesema ushauri huo umefuatia utafiti walioufanya na kubaini kuwa kuna watu wengi ulemavu ambao wanafungiwa ndani na wazazi wao tangu wakiwa wachanga, kwa kuogopa kuchekwa na watu katika jamii zao.

Amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kwamba vimekuwa vikiwanyima fursa ya kupata haki elimu walemavu hao.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.