11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

TASAF watumia shilingi milioni 9.5 Kisarawe
 
2008-05-11 20:02:27
Na Radio One Habari

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF, wilayani Kisarawe, umetumia shilingi milioni 9.5 kusaidia mradi wa kilimo cha ufuta na karanga, kwa vikundi viwili vya wazee katika tarafa ya Mzenga wilayani humo.

Mratibu wa Mfuko huo wilayani Kisarawe, Bwana Desideri Mulagala, amesema mfuko huo umefadhili mradi huo, kufuatia azma ya wilaya ya kuwa na mazao mbadala ya biashara badala ya kutegemea korosho pekee.

Amesema wilaya hiyo pia imeazimia kulima pamba na alizeti, baada ya utafiti kubaini kuwa yanaweza kustawi kama ilivyo katika mikoa mingine nchini inayolima mazao hayo.

Bwana Mulagala amesema kikundi cha wazee kijiji cha Chakenge tarafa hiyo ya Mzenga msimu wa mwaka 2007 walivuna kuvuna kilo 5, 830 za karanga ambazo waliuza na kujipatia shilingi milioni 6.3.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.