11 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Daraja la Kiteputepu limeanza kuharibika
 
2008-05-11 20:01:56
Na Radio One Habari

Daraja la Kiteputepu linalounganisha wilaya za Sumbawanga na Mbozi limeanza kuharibika, hivyo kuzusha wasiwasi kwa watumiaji na kuzorotesha usafirishaji wa mazao kutoka mashambani na mifugo.

Pamoja na kuelezea wasiwasi huo, wakaazi wa wilaya hiyo waishio karibu na daraja hilo wametaka hatua zichukuliwe kudhibiti matukio ya uhalifu eneo hilo kwani wahalifu huwavizia watu usiku na kuwakaba na wengine kutoswa mtoni ili kupoteza ushahidi hasa nyakati za shughuli za minada.

Msimamizi wa kivuko hicho Bwana Magogo Sanga amesema daraja hilo lililojengwa na Kanisa Katoliki mwaka 1995, limekuwa msaada mkubwa kuunganisha pande mbili za mikoa ya Mbeya na Rukwa ambapo wastani wa watu elfu mbili hutumia kwa siku.

Hata hivyo Bwana Sanga amesema nguvu ya serikali inahitajika katika kuliimarisha badala ya kuliachia kanisa liendelee kukikarabati.

Tathmini iliyofanywa na wakala wa barabara TANROADS, imeonesha kuwa ujenzi wa daraja la kuunganisha mikoa miwili ya Rukwa na Mbeya kupitia barabara ya Kamsamba ungegharimu zaidi ya shilingi bilion tatu.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.