|
Wanaouza mafuta ya petroli na dizeli kinyume cha sheria kusakwa Z`bar
2008-05-11 20:00:45
Na Radio One Habari
Bodi ya Mapato Zanzibar-ZRB kwa kushirikiana na jeshi la polisi katika mkoa wa Mjini na Magharibi imeanzisha operesheni maalum kuwasaka wauzaji wa mafuta ya petroli na dizeli kinyume cha sheria katika manispaa ya Zanzibar.
Kamanda wa polisi wa mkoa huo Bwana Bakari Khatibu Shabani amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema polisi na bodi hiyo zimeanzisha operesheni hiyo kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kuanzisha utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo sehemu ambazo hazikubaliki kisheria na kuhatarisha maisha.
Kamanda Bakari amesema sababu nyingine ni kupambana na wafanybiashara ambao wanaikosesha serikali kodi inayotokana na uuzaji wa mafuta.
Amesema wafanyabiashara kadhaa wamekamatwa tangu kuanza oparesheni hiyo na kwamba itaendelea.
|