10 May 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Uendeshaji wa Mashamba ya mpunga ya Kapunga uratibiwe
 
2008-05-10 19:26:52
Na Radio One Habari

Serikali imeombwa kuratibu uendeshaji wa mashamba ya mpunga ya Kapunga Mkoani Mbeya ambayo wamiliki wake wanataka kulima zao la mibono kwa ajili ya kuzalisha nishati ya kuendeshea mitambo badala ya kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

Wakizungumza baada ya kutembelea mashamba ya miwa ya Kilombero na bwawa la uzalishaji wa umeme la Kidatu, wajumbe wa Bodi ya maji ya Bonde la Rufiji wamesema hatua ya mwekezaji kubadili kilimo cha mpunga ambalo ni zao la chakula na kulima mibono kitapunguza upatikanaji wa chakula.

Makamu mwenyekiti wa bodi bwana Abed Mwasajone amepinga uamuzi huo na kusisitiza kama mwekezaji ameshindwa kulima mpunga serikali ichukue mashamba hayo na kugawa kwa wananchi.

Hoja hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wa bodi hiyo bwana Bakari Mbonde ambae amesema hatua hiyo itakuwa na athari kubwa kimazingira na mtiririko wa maji katika bonde la Ihefu na mto Ruaha mkuu.

Kwa siku za karibuni wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni kuwa ujio wa kilimo cha mazao yanayolenga kuzalisha nishati ya kuendeshea mitambo utaathiri uzalishaji wa chakula na hifadhi ya mazingira kwani kilimo hicho kitahitaji maeneo makubwa na kuhusisha ufyekaji wa misitu na mapori.


  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.