19 Mar 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Ajali ya basi yauwa watu wanne Dodoma
 
2008-03-19 17:41:25
Na Radio One Habari

Watu wanne wamekufa papo na wengine 18 kujeruhiwa baada ya basi la Champion linalofanya safari zake kati ya Dodoma na Dar es Salaam, kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa pembeni mwa barabara katika wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.

Waliokufa katika ajali hiyo wametajwa kuwa ni Brasius Mtei, kondakta wa basi Ramadhani Kinyausi, Mohamed Hussein, na utingo wa basi hilo Omary Kitija wote wakazi wa Mkoa wa Dodoma.

Ajali hiyo ilitokea jana saa mbili usiku katika Kijiji cha Silwa, kata ya Pandambili wilayani Kongwa, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 710 ADR kuligonga lori lenye namba za usajili T 754 ARS.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bwana Omary Mganga amesema basi hilo lilikuwa likienda Dodoma kutoka Dar es salaam likiwa na abiria 36 na kwamba kati ya abiria hao 18, tisa wamepata matibabu na kuruhusiwa na wengine 9 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa kwa Dodoma.

Baadhi ya majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wamesema sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi pamoja na taa za basi hilo kuwa mbovu na hivyo kutoa mwanga hafifu.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Dakta Frida Mokiti amesema majeruhi hao wanaendelea vizuri na matibabu.

  • SOURCE: Radio One
Tuma Maoni Yako
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.