08 Feb 2008 MAIN PAGE SITE INDEX CONTACT US HELP
  Swahilinews
NAVIGATION
SEARCH
 
SPECIAL  
ARCHIVES  
Print this article Send this article

Zaidi ya shilingi bilioni 3 kusaidia asasi zisizo za kiserikali
 
2008-02-08 17:08:28
Na Radio One Habari

Zaidi ya shilingi bilioni tatu zimetengwa kutumika katika kuendeleza mradi wa kuzisaidia asasi zisizokuwa za kiserikali katika kukabiliana na changamoto za kuleta maendeleo na kupunguza umaskini.

Mratibu wa mradi huo Avence Mori amesema hayo mjini Zanznibar katika warsha ya kujadili Mpango na Sera ya Kuondoa Umaskini Zanznibar-Mkuza kwa taasisi zisizokuwa za kiserikali.

Amesema mradi huo wa miaka 3 unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya muungano na Jumuia ya Ulaya kufuatia mkataba wa Cotonou unaolenga kuatoa nafasi za maendeleo kwa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific.

MORI amesema tathmini zilizofanywa zimeonesha kuwa iwapo miradi midogo midogo itasaidiwa vilivyo inaweza kupunguza umaskini kwa asilimia kubwa.

Hata hivyo amesema mradi huo utaweza kutekelezwa kwa ushirikiano na viongozi ikiwemo kuratibu shughuli za mradi pamoja na kuwasilisha ripoti makao makuu ya mradi.

  • SOURCE: Radio One
Habari za Leo
-----------------------------------------------
Maoni ya Mhariri
-----------------------------------------------
Business bits
-----------------------------------------------
Makala
 
Privacy Statement Terms Of Use ©1998-2007 IPPMedia Ltd.  All Rights Reserved.